Katika makala haya shaba yetu inalenga nchini DRC hasa eneo la Mashariki, ambapo tunajadili haki za malemavu eneo hilo. Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamia ya watu wenye ulemavu wamejikuta wakihangaika kuokoa maisha yao, kipindi hiki vita vikiendelea kusheheni eneo hilo. Miji kama Goma, Rutshuru na Sake imeshuhudia maelfu wakikimbia maakazi yao. Lakini kwa wengi wenye ulemavu, kukimbia si jambo rahisi. Wengine wanatembea kwa magongo, wengine hutumia viti vya magurudumu ambavyo haviwezi kuvuka matope, milima, au mabonde. Skiza makala haya kufahamu mengi
--------
--------
Uganda : Uchaguzi raia wanafahamu haki zao
Uchaguzi nchini Uganda, unatarajiwa kufanyika mwezi January, Rais Museveni akichuana tena na Hasimu wake wa kisiasa mwanamziki aliyeukia siasa, Bobi Wine. Skiza makala haya kufahamu mengi.
--------
--------
Kenya/Nigeria : Wanawake wanahangaishwa kwa mitandao
Katika makala haya tunaangazia suala linalozidi kuwa pasua kichwa—unyanyasaji wa wanawake kwenye mitandao ya kijamii. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na shirikisho la mawakili wanawake nchini Kenya FIDA, kwa ushirkiano na wenzao wa kutoka nchini Nigeria, unaonesha kuwa karibu kila mwanamke anayetumia mitandao amewahi kushambuliwa iwe ni kwa maneno ya matusi, vitisho, au kusambaziwa picha binafsi bila idhini yake. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
--------
--------
DRC : Unyanyasaji wa haki za watoto
Watoto wanatumika kwa baishara ya ngono Skiza makala haya kufahamu mingi zaidi
--------
--------
À propos de Jua Haki Zako
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.